Mpango Wa Mungu Wa Nyakati

 

      Historia ya mwanadamu imejawa na dhiki na maombolezo. Bali haitakuwa hivyo daima. Mungu ameahidi, ingawa “Kilio huja kukaa usiku, asubuhi huwa furaha.” Zab. 30:5. Naam, badala ya enzi hii ya dhambi, kutakuwa na enzi mpya ya furaha kwa watu wote idumuyo milele.

“Kilio huja kukaa usiku, asubuhi huwa furaha.” Zab. 30:5.

 

     Je yawezekana tuamini ahadi za Mungu? Hakika yawezekana! Kuna mengi Duniani na katika Biblia yaonyeshayo ule ukweli wa Neno la Mungu. Utaratibu wa nyota na dunia ya kupendeza iliyo makazi ya mwanadamu, ni ushahidi tosha wa Muumba mwenye ufahamu na uweza. 

     Ufumbuzi katika magofu na mahame ya miji ya kale umedhibitisha kuwa historia ya Biblia ni sahihi. Sheria aliopewa Musa imedhibitishwa kuwa haki na hivyo imenakiliwa pakubwa na mataifa mengi duniani. Yaajabisha jinsi ubashiri wa biblia ulivyo wa kweli. Waisraeli warudi kwenye Nchi ya ahadi. (Yer. 16:14-16, Amosi 9:14-15) ulimwengu wote wajiandaa kwa vita (Yoeli 3:9-10, Mat. 24:6-7) vitakavyo sababisha nyakati za dhiki ambayo haikushuhudiwa tangu mwanzo (Mat. 24:21-22, 2 Tim. 3:1-4) maarifa ya ulimwengu yaongezeka kwa kasi; ilhali maarifa ya kweli ya Mungu ni nadra sana huyapata (Dan. 12:4, Amosi 8:11-12). Haya yote yatendeka leo. Hii yatupa ujasiri katika Biblia na katika ahadi za Mungu zijazo.

Ramani ya nyakati

     Biblia yatwambia kuwa Mungu, Baba wa Mbinguni, Atupenda kila mmoja wetu kwa upendo mkuu kama wanawe. Upendo huu ni dhahiri katika mpango wa ajabu wa wokovu aliyopanga.

     Tunapozidi kuujua, ndivyo tuonavyo wema wa Mungu na upendo wake kuhusu watu wote wakila rangi, kabila na lugha Mpango wa Mungu ni taratibu na unaendelea. Ni kama ramani iliyochorwa na mjenzi mkuu hata kabla ya dunia kuumbwa. Kupitia kwa nabii Habakuki, Mungu alisema kuwa jonzi ya mpango wa wokovu ingeliandikwa kwa ramani na kuwekwa wazi. (Hab. 2:2,13) Ramani ya nyakati yaonyesha utaratibu wa mpango huo, kwa kutumia mchoro wenye ishara kuonyesha yaliyomo. Kwa mkhutasari, ramani hii yatangulia kuonyesha atakayotenda Mungu katika kurejesha mwanadamu kwenye ukamilifu wa Edeni uliyopotea, na kuwaita wateule wachache ili kumsaidia Yesu kubariki watu wote.

nyakati na majira

     Katika 2 Tim. 2:15, Mtume Paulo atuhimiza kulisoma Neno la Mungu ili tujionyeshe kuwa tumekubaliwa na Mungu, tukitumia kwa halali Neno la kweli. Hili ndilo jambo la kwanza ambalo Ramani ya Nyakati yatusaidia kufanya. Zile duara—dufu zilizo juu ya ramani husaidia kugawanya nyakati za historia ya mwanadamu duniani, ziitwazo dunia. Tukisha fahamu maumbo haya ya nyakati, ni rahisi kuanisha maandiko mengi katika Biblia yaonekanayo kuhitilafiana.

     Hizi dunia tatu zaonyeshwa kutoka kulia hadi kushoto juu ya ile ramani; zarejelewa mara kwa mara katika Maandiko** “A” yaitwa na Petro “ulimwengu uliyokuwepo”; “B” na Paulo “ulimwengu mwovu wa sasa”; na “C” “ulimwengu ujao.” Ulimwengu wa kwanza ulidumu tokea kuumbwa mwanadamu hadi ile gharika; wa pili kutoka hiyo gharika hadi mwanzo wa utawala wa Miaka Elfu wa Kristo na watatu tokea hapo hadi milele Yote. Majira na nyakati “B” na “C” yamegawanywa kwa vizazi, ambavyo yafafanua zaidi zile hatua za Mpango wa Kiungu na maelezo zaidi ya mapenzi ya Mungu.

 

CHDispensationsA.gif (9253 bytes)

“D”

      “D” ni kizazi cha wazee wa imani alichonusurika Nuhu na walichoishi Ayubu, Abraham, Isaka na Yakobo. Mengi waliopitia yalikuwa ni mifano* ama ishara ya mambo yajayo. 

“E”

TABPriestsSacrificing.jpg (3312 bytes)TabPriestBull.jpg (4327 bytes)

     “E” ni Enzi ya Wayahudi kuanzia kifo cha Yakobo hadi wakati wa Kristo. Huu ni wakati ambao taifa la Kiyahudi lilipata kibali hasa machoni pa Mungu kama wateule wake.

     Lile Agano* la Sheria, lilifanywa kwao. Pia waliambiwa watengwe na mataifa yaliyo wazingira ya wasio amini. Israeli pia alikuwa ni mfano wa mambo yajayo.—1 Kor. 10:11.

 

“F”

Jesus12Praying.jpg (2325 bytes)

      “F” ni Wakati wa Injili ambao Kanisa*, yaani mwili wa Kristo, waitwa watoke ulimwenguni. Wao ni “Mwito mkuu” kuendea utukufu, adhama na kutokuharibika,” waridhi wa asili ya kiungu.

    Huku wakipambana kuufanya mwito wao Na uteuzi kuwa wa hakika, uovu umeruhusiwa kutawala ulimwengu ili kuujaribu uaminifu wao. Hao pekee ndiyo waliojitoa ili kuteseka pamoja na Yesu na kutoa uhai wao kwa Mungu katika ulimwengu wa wasioamini, wafaa kushiriki na Yesu katika utawala wake wa utukufu.

“G”

TIChild1.jpg (15520 bytes)

      “G” ni utawala wa miaka Elfu wa Kristo na kanisa, kusudi kuangusha maadui wote wa Mungu huku jamii zote za dunia zikibarikiwa. Petro anena kuhusu nyakati hizi, “nyakati za kurejeshwa” kwa mambo yote, zilizonenwa zamani kwa vinywa vya manabii watakatifu wa Mungu. (Matendo 3:21) 

    Huu ndiyo wakati wa kurejesha hali kamili ya paradiso, kuimarisha amani, njaa na uhaba kuondolewa, na kutakuwa na “wakati mfupi” wa kujaribwa (Ufu. 20:7-10, ambapo shetani na watendao dhambi makusudi wataangamizwa katika mauti ya pili, nakuacha dunia ya uzuri na amani. Kisha kutakuwa na mwanzo wa enzi ijayo.

    “H”, idumuyo pasina mwisho: Enzi ya ukamilifu, baraka na furaha kwa wote.

    Mwisho wa nyakati za Wayahudi na Injili wajulikana kama “Mavuno,” ambapo pana utimilifu wa kazi za nyakati hizo mbili. Katika mavuno ya Nyakati za Wayahudi, “waisraeli wachache sana”—ngano ya kweliwalitengwa na kapi, kabla taifa la Israeli kuharibiwa, katika maangamizi ya Yerusalemu. Vilevile mwishoni mwa Nyakati za Injili, wateule wa Mungu—ngano ya kweli—watengwa na magugu, huku nyakati za taabu zilizo tabiriwa, zikiangamiza hali potovu ya jamii iliyopo sasa, kuandaa njia ya Ufalme wa Kristo.

Hatua za Kufikia Utukufu

    Katika ile Ramani, mwendelezo wa nyakati waonekana kutoka kushoto hadi kulia. Pia utatambua kuwa kuna mistari kadhaa ionyeshayo viwango, iliyo na herufi ziitwazo “viwango” Hii yawakilisha aina ya maisha ya kimsingi na hatua za kuyafikia. “N” ni kiwango cha kibali cha Mungu. Yajumlisha utu mkamilifu, hali isiyo ya dhambi iliyokuwa na Adamu kabla kuanguka.

    Alipokaidi Mungu, alianguka hadi kiwango cha dhambi “X.” Tokea hapo kuendelea ulimwengu wote upo kiwango “M,” kwa kuwa wote wamehukumiwa kupitia Adamu.

Baptism1.jpg (2649 bytes)

    “N” ni kiwango kilichomilikiwa na wamwendeao Mungu, wavutwao naye kwa imani katika Yesu. Wakiendelea hivyo na kutoa yote na maisha yao kuwa dhabihu, Mungu huwahesabia haki* kikamilifu. Awahesabia kuwa watakatifu huru toka dhambini. Wastahili kwa sababu Yesu astahili. Hawa pia waonyeshwa katika kiwango “C,” kiwango cha kuzaliwa kiroho. Hali ya kuzaliwa na Roho wa Mungu kuwa kiumbe kipya. Licha ya kuwa wanadamu, Mungu hawahesabii hivyo machoni mwake, ila ni wa kiroho, kwa maana utu wao umehesabiwa kutolewa dhabihu na kutupiliwa mbali. Wamefanyika “viumbe vipya katika Kristo Yesu. Matumaini na mapenzi yao ya kale yametolewa kwake Yesu.

    Hiki ni kiwango ambacho wafuasi wa kweli wa Yesu watambuliwa katika maisha ya sasa.

    “K”

CrossCrown2.jpg (8427 bytes)

     Ila ni jambo moja kufanya agano na Mungu ili kuishi maisha ya utaua na pili kuishi hilo agano hadi kufa. Watakaomwamini watafufuliwa katika kiwango “K,” kiwakilishacho hali ya uzazi wa kiroho.

    Hiki ni kiingilio halisi cha maisha kama kiumbe cha kiroho, ambapo wachukua umbo la malaika ilhali uweza na asilia yao ni ya kiwango cha juu kuliko wanadamu.

    Hatua zaidi na iliyo kuu sana awezayo kuiga mtu, ni kwango “D,” ambacho ni utukufu wa cheo au daraja, isiyo tu kubadilishwa kiumbe cha kiroho ila kuketi katika kiti cha Enzi cha Yesu, kuinuliwa kuketi pamoja naye kwenye mkono wa kulia wa Mungu Mwenyezi.

VYEO VYA WATU

    Taswira nyingine kwenye hii ramani ni matumizi ya piramidi ili kuwakilisha watu fulani maarufu katika Maandiko na vyeo mbalimbali vya watu. Adamu angali mtu mkamilifu kabla kutenda dhambi, aonyeshwa kwa piramidi ndogo iliyo kamilika, “a” chini yake ni “b” isiyo kamili, isiyo na kifuniko, ikiashiria ulimwengu wa wanadamu usiyo kamilika kabla ya gharika, uliyoharibiwa na dhambi, C  d yaendeleza hii taswira, uliyoharibiwa na dhambi, “d” aendeleza hii taswira ya watenda dhambi, wakiongezeka kwa idadi baada ya ile gharika hadi kazi ya ile miaka Elfu ianzapo.

    Piramidi ndogo ya “c” yaonyesha Ibrahimu na wastahiki wengine aliyowafanya wapenzi wake Munguwenye haki machoni mwake.

    Ingawa hawakukamilika, walihesabiwa haki kwa imani yao kuu. Wlikuwa kinyume sana na watenda dhambi wa “R” ambao ni maadui wa Mungu kwa sababu ya kazi zao mbovu. Piramidi “e” yawakilisha Israeli taifa katia Enzi ya Wayahudi, ambapo sadaka za wanyama zilikubaliwa na Mungu kama mifano ya tambiko ya dhambi za taifa.

    Utaratibu huu wa sadaka za wanyama chini ya sheria ya Musa, haukufidia dhambi za watu kikamilifu, ila uliashiria dhabihu halisi ya Kristo iondoayo dhambi za watu kabisa.

    Kwa hiyo Israeli ya kimwili yaonyeshwa katika kiwango “P,” E yaani mfano wa kuhesabiwa haki. Piramidi ndogo “g,” P “h,” “i,” “k,” na “l,” zote zaonyesha picha ya Yesu. Akiwa na umri wa miaka 30, mtu mkamilifu (“g”). Alibatizwa katika Mto Yordani, apakwa mafuta na Roho wa Mungu, na kuzaliwa hadi kiwango cha “M” (piramidi “h”).

Jesus35BaptismA.jpg (9196 bytes)

    Kwa hiyo kwa miaka 3 ˝ aliyatoa maisha yake ya kibinadamu huku akiwafunza wanadamu kuhusu Mungu na ule ufalme ujao. Aliponya wagojwa huku akiwaita wanafunzi wamjie. Huduma yake ilimalizikia Kalvari katika mauti, iyonyeshwayo kwenye kiwango “N,” Kwa msalaba, alipojitoa kama fidia* Kwa ajili ya uasi wa Adamu.

    Hili lilikuwa ni tukio la kipekee sana lililowahi kutukia katika historia ya mwanadumu duniani. Yatufanya kushuruku daima. Kwa maana matumaini yote ya maisha yajayo yategemea uhuru kutoka kwa adhabu ya Adamu kwa ustahiki wa sadaka na fidia aliyotoa Kristo.

    Baada ya kuwa mautini kwa siku tatu, Yesu alifufuliwa mwenye upya wa maisha katika kiwango “L,” alipozaliwa kwa Roho (“I”), mfano wa malimbuka ya waliokufa. Kwa siku arobaini alijionyesha kwa wanafunzi wake huku akiwahimiza na kuwadhibtisha. Kisha akapaa kwa utukufu, Roho iliyofufuliwa. Hiki ni kiwango cha juu sana (cha kiungu) cha kuishi, yaani kiwango “K,” kinachoonyeshwa kwa piramidi ndogo “k” na “l”. Kuja Kwa Pili kwa Kristo karibu na mwisho wa Nyakati za Injili kwaonyeshwa kwa “r” kabla hajatukuzwa machoni pa ulimwengu. Kwenye Mavuno ya Nyakati za Injili, aungana na washindi waaminifu, wafuatao hatua zake, (“s”).

    Pamoja, wajumlisha kimo cha Kristo, Kichwa na Mwili, katika piramidi “w”kwa mavuno, na kwa “x”, akitawala kwenye utukufu katika Enzi ya Miaka Elfu.

     Hebu sasa tazama ile piramidi kubwa isiokamilika inayoporomoka katika Nyakati za Injili, katika mavuno ya nyakati zile.

      Yawakilisha madhehebu yote kwa jumla ambayo yadai kuwa mwili wa Kristo, Utatambua kuwa sehemu “n” na “m” zote mbili ziko katika uzawa wa kiroho wa kiwango “M”; Hawa nao wawakilisha wafanyikao Bibi Arusi wa Kristo na lile Kundi Kubwa, mwandamo. Ni daraja la Bibi Arusi pekee (“n”) lililoaminika kikamilifu kwa agano lake na hivyo huushinda ulimwengu, mwili, na shetani. Hawa ni “Kundi Ndogo” ambalo ilimpendeza Baba kuwapa viwango vya heshima (piramidi “x”) katika Ufalme wa Mbinguni. Lile kundi kubwa “m” huanguka na kushindwa kutimiza lile agano na hivyo, hupoteza haki ya kufikia kiwango “K,” kiti cha enzi na utukufu; walakini Mungu angali awapenda na atawapa vyeo vya madaraka ya chini, kiwango “L” (piramidi “y”) katika Ufalme wa Mbinguni.

      Sehemu “p” yawakilisha kundi kubwa la madhehebu ya dini, yaonyeshwayo katika kiwango “N”; wahesabiwa kuwa katika kiwango cha juu wakilinganishwa na ulimwengu wa dhambi, kwa sababu, kwa kiasi Fulani waamini kazi aliyotenda Yesu. Hata hivyo hawakuweza kuendelea, kwa sababu walishindwa kuyatoa yote waliyo nayo kwa huduma ya Mungu, hawakuzaliwa na Roho wala hawakuhesabiwa haki na hivyo hawaonekani katika kiwango “M.” Katika ufufuo, hii tabaka, sehemu ya “W” katika piramidi ya enzi ya Milki ya Miaka Elfu, watafufuliwa wenye uhai wa wanadamu.

      Hapo wataendelea Kwa upesi, kuufikia ukamilifu, huku wakifurahia ule ufalme hapa duniani, na heshima yake.

      Sehemu “q” yawakilisha tabaka iliyochanganyika na madhehebu ya dini ila hawakfumwamini Yesu.

      Wao ni “mbweha wavaliao ngozi ya kondoo,” wala hawana sehemu yoyote katika kanisa, kwani wameliumiza sana. Wote ni magugu (“v”) ya ule mfano yatakayo chomwa katika Mavuno, ingawa wote watafufuliwa katika ule ufufuo wa wote na kuwapa fursa ya kupata uzima wa milele wakifunzwa katika haki.

      Sehemu ya “S,” iliyo na uvuli, yawakilisha wakati wa dhiki duniani katika Mavuno ya Injili, ambapo makundi mbali mbali ya madhehebu, “u” na “v,” yavunjika vipande vipande. Lile Kundi Kubwa (“t”) lashindwa kupata ile dhawabu kuu. Ni lile Kundi Ndogo tu (“s”), ngano ya kweli iliyoiva, liwezalo kujitenga na madhehebu na unajisi wake, ayaitayo Bwana “Babiloni,” au utatanisho.

DHAWABU NA MAJUKUMU

      Katika picha kamili ya Milki ya Miaka Elfu, ionyeshwayo kwa piramidi kubwa iliyo kamili, vyeo vyote vinne vya watu watakaopita uzima wa milele, vyaonyeshwa. Pale juu ni Kanisa na lile Kundi Kuu (“x” na “y”), yote kwa viwango vya kiroho, kama ilivyoelezwa awali. Chini yake, katika kiwango cha watu wakamilifu, ni Israeli ikiwa taifa maarufu lililorejeshwa (“z”), hali wanadamu waliosalia (“W”), jamii zote za dunia, wakiinuliwa na kupana na Mungu. Waovu wote watakapoharibiwa, katika Mauti ya Pili, Mpango Mkuu wa Mungu wa Nyakati utatimizwa kabisa. Hapo ndipo yatatimizwa maneno haya yaliyobarikiwa, “wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio. . . kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” Ufunuo 21:4.

PyramidEstelleB.gif (33871 bytes)

      Lo, huu ni mpango mkuu jinsi gani! Ulio na utimilifu wa upendo wake Baba. Ila fursa ya kuelewa mpango wa Mungu ina jukumu pia.

      Lo, huu ni mpango mkuu jinsi gani! Ulio na utimilifu wa upendo wake Baba.

      Ila fursa ya kuelewa mpango wa Mungu ina jukumu pia. Mungu awaita wale wanaojitambua na kujitoa kwake, walio na bidii ya Neno, kwa kukua katika neema na ujuzi na kuitangaza Injili* ya Ufalme kwa wengine.

      Na tuupokee mwito wa Mungu, tuhesabu garama, na kwa msaada wake, tuingie katika njia ya ushindani iongozayo hadi uzima wa milele pamoja na Mwokozi wetu.

      Tukiwa waaminifu, tutapata fursa ya kubariki watu wote duaniani na kuleta sifa na utukufu kwa Baba yetu aliye Mbinguni.

ORODHA YA MAJINA KANISA—mwili wa waaminio, waliyoitwa kutoka ulimwengu ili kumfuata Yesu.

KUFANYWA WAKFU—Kujitoa kabisa Kwa Mungu, kujitoa dhabihu kwa huduma ya ukristo. Lawi 8:30; Math. 16:24.

AGANO—Mkataba wenye uchaji, aghlabu kati ya Mungu na mwanadamu.

INJILI—Habari Njema, hasa ya wokovu wa Kristo na ya baraka zijazo za Ufalme wa Mungu.

KUHESABIWA HAKI—Ni kitendo cha neema kutoka kwa Mungu akimhesabia mwenye dhambi kuwa ana haki machoni mwake mbali na hukumu ya Adamu. Rum. 5:1-9

FIDIA—Garama halisi iliyo sawa. Dhabihu aliyotoa Yesu badala ya Adamu, itakayowafanya huru wanadamu kutoka mautini 1 Tim. 2:5-6.

KUREJESHA—Kurudisha, kurejea kwa hali ya awali iliyokuwa imepotea Matendo 3:21.

MFANO—Utaratibu au utangulizi wa jambo kuu lijalo kwa mfano Ibrahimu akimtoa Isaka mwanawe ni mfano wa Mungu akimtoa mwanawe Yesu kuwa dhabihu.

      Pia tunayo: mpango wa Mungu wa nyakati Biblia ni kweli. Ila tutaielewaje? Kila andiko linapopatana, basi twajua kuwa tuna ukweli kuhusu somo Fulani, Kitabu, “MPANGO WA MUNGU WA NYAKATI,” huonyesha jinsi ya kupatanisha maandiiko. Hujumlisha maelezo ya kilindi ya ile Ramani ya nyakati. Yaonyesha mwandishi wa Biblia kuwa Mungu mwenye hekima haki upendo na uwezo.

To Return to Home Page click on Chart.
 
        

Email
with questions
or comments
about this web site.